
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limejipanga kikamilifu katika
kuhakikisha Maadhimisho ya sikukuu katika kipindi hiki cha mwisho wa
mwaka 2015 na mwanzo wa mwaka 2016. Siku kuu zinazotarajiwa ni Mkesha wa
X- Mass katika Makanisa mbalimbali hadi siku yenyewe ya X- Mass tarehe
25/12/2015 na hatimaye tarehe 01/01/2016 Sikukuu ya mwaka mpya.

Jeshi hilo limesema litaimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali
ya biashara na mikusanyiko ya watu kwa kushirikiana na vyombo vingine
vya dola ili kuhakikisha yeyote mwenye nia ovu ya kufanya uhalifu wa
aina yeyote anadhibitiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Baadhi ya askari polisi mjini Dodoma wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Afande Mambea.