Kanisa moja mjini Berlin limetangaza kwamba litaandaa ibada maalum kabla ya Krismasi itakayoongozwa na filamu ya Star Wars.
Kuna
msisimko mkubwa Ujerumani kabla ya kuzinduliwa nchini humo kwa filamu
mpya ya mwendelezo wa filamu za Stars Wars kwa jina The Force Awakens
Alhamisi.
Kanisa la Zion Church, lililoko eneo la katikati mwa
jiji la Mitte, limetumia msisimko huo kuandaa ibada ya kipekee ya
Jumapili asubuhi.
Ibada hiyo itaongozwa na filamu nambari nne ya Star Wars kwa jina Return of the Jedi.
Filamu hiyo ilizinduliwa mwaka 1983, na wale watakaohudhuria ibada hiyo wataonyesha sehemu za filamu hiyo.
Wazo la kuandaa
ibada hiyo lilitokana na wahubiri wawili ambao wanajifunza kuhubiri,
Ulrike Garve na Lucas Ludewig, kanisa hilo limesema kwenye tovuti yake.
Wanalinganisha filamu hiyo ya George Lucas na matukio kwenye Biblia.
“Katika
tukio moja Luke Skywalker ianavutwa upande wa mfalme, wa maovu,”
anasema Ludewig, ambaye ameelezwa na kanisa hilo kuwa mwanatheolojia na
mtaalamu wa Star Wars.
"Luke anapinga kwa kusema: Sitawahi kujiunga na upande wa giza.”
Hilo
anasema linalingana na sehemu kwenye kitabu cha Warumi: “Msiruhusu
maovu yawatawale, lakini shindeni uovu kwa kutenda mema.”
Bi Garve anasema wale watakaotokea wakiwa wamevalia
mavazi sawa na yanayovaliwa kwenye filamu hizo ana nafasi ya kuingizwa
kwenye shindano la kushindania tiketi za kutazama filamu ya sasa ya The
Force Awakens.
Nchini Kenya, filamu hiyo mpya ya Star Wars inatarajiwa kuanza kuonyeshwa Kenya Desemba 18.