Matokeo ya utafiti uliofanywa na
shirika la kijamii la Twaweza yanaonesha zaidi ya 80% ya Watanzania
wanaona nchi yao iko salama kutoka kwa vitendo vya makundi yenye itikadi
kali.
Utafiti huo wa maoni ulifanywa kati ya mwezi Septemba na
Oktoba mwaka huu ukitaka kujua mtazamo wa wananchi juu ya hali ya
vitendo vya itikadi kali nchini.
Kwa mujibu wa utafiti huo, ingawa
wananchi wengi wanajihisi kuwa salama, takribani asilimia 56 wana
wasiwasi juu ya vitisho vya mashambuliz dhidi ya Tanzania katika siku
zijazo.
Hata hivyo Meja Jenerali Venansi Mabeo, ambaye ni mkuu wa
usalama katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi la Tanzania ameondoa wasiwasi
huo na kusema hali ya usalama si ya kutia shaka.
Wakizungumzia
sababu zinazowashawishi watu wengi kuvutiwa na itikadi hizi, wananchi
wengi wamesema ukosefu wa ajira, utawala mbovu pamoja na kukatishwa
tamaa na mifumo ya serikali ni mambo yanayoongoza katika ushawishi huo
Kwa
upande mwingine, wananchi katika ripoti hiyo wamesema wanapendelea
zaidi njia ya kijeshi kuliko ya mazungumzo katika kupambana na vikundi
hivi vyenye itikadi kali
Huku zaidi ya asilimia 90 wakionyesha
kuridhishwa kwao na vyombo vya ulinzi na usalama na kusema wana Imani
kwamba vinaweza kuwalinda dhidi ya vitisho vya mashambulizi
Mkurugenzi
Mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze amesema hata kama utafiti huu unahusu
hisia pekee za wananchi, unasaidia pia katika kutoa picha ya juhudi za
serikali katika kuimarisha hali ya usalama miongoni mwa wananchi.
Mwandishi
wa BBC Sammy Awami anasema tangu shambulio la ubalozi wa Marekani
jijini Dar es Salaam mnamo mwaka 1998, Tanzania imeonekana kukwepa balaa
la mashambulizi ya kigaidi.
Ripoti hiyo ya Twaweza inasema Tanzania imo katika nafasi nzuri ya kutafuta njia