Daktari akifanya upasuaji wa uume.kijana mmoja wa miaka 17 nchini Uingereza amefanyiwa upasuaji kupunguza uume wake.
Mvulana mmoja amefanyiwa kile madaktari wanasema ni upasuaji wa kwanza wa kupunguza uume wake.
Kijana
huyo wa miaka 17 alikuwa akilalamika kwamba hangeweza kushiriki katika
tendo la ngono ama hata kushiriki katika michezo swala lililomshinikiza
kuomba kupunguzwa uume wake.
Kabla ya kufanyiwa upasuaji huo uume huo ulikuwa na urefu wa inchi 7 na mzingo wa inchi 10.
Daktari
wa upasuaji Rafael Carrion kutoka chuo kikuu cha Florida kusini ambaye
alifanya upasuaji huo aliliambia gazeti la Mail Online la Uingereza
kwamba ''kuna wakati ambapo kila daktari wa upasuaji hupata ombi la
maajabu linalokuacha kinywa wazi.
''Swali hilo ni je, unaweza kuufanya uume wangu kuwa mdogo?".
Kwa wale waliohitaji kufanyiwa upasuaji huo, uume wao hauwi mkubwa wakati unapodinda bali huwa mgumu.
Daktari huyo alisema kwamba wengu hufanyiwa upasuaji wa kukiongeza kiungo hicho na wala si kukipunguza.
Kijana huyo alifanyiwa matibabu hayo na kumaliza matatizo yake.