Benki Kuu ya Marekani imepandisha kiwango kikuu cha riba kwa alama ya robo ya asilimia.
Kwa muda wote tangu mtikisiko wa uchumi nchini humo mwaka 2008 riba ilibaki kuwa asilimia sifuri.
Imekuwa
ni kipindi kisicho cha kawaida katika sera za uchumi nchini Marekani na
sasa hatua ya benki kuu imeweka alama ya kuanza kurejea kwa kiwango cha
riba cha kawaida.
Imechukua takriban miaka saba kwa Benki hiyo
kuchukua uamuzi huo wa kuongeza kiwango hicho kidogo cha riba. Hii ni
sehemu ya kujikinga na hatari ya mfumuko wa bei kwa siku zinazokuja.
Hata hivyo hatua hiyo sasa inatia mashaka kwa uchumi wa nchi zinakuwa kwa haraka kama Uturuki, Brazili na Afrika Kusini.
Kuna
uwezekano kuwa uamuzi huo sasa utawafanya baadhi ya wawekezaji kuondoa
fedha zao ili kufaidika na riba hiyo kubwa nchini Marekani.
Pia hatua hiyo itadhoofisha sarafu ya nchi hizo na kuongeza gharama za mikopo.
Aidha
pia hatua inatarajiwa kuyumbisha mfumo wa fedha japo nchi tajiri
zinaweza kuimarika zaidi kama zitahimilli msukuko huo tafauti na hapo
awali.