
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na
Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Jeshi la Polisi katika Ukumbi wa Mikutano
wa Kituo Kikuu cha Polisi (Central) wakati alipokitembelea kituo hicho
cha Polisi jijini Dar es Salaam leo. Pia Waziri Kitwanga katika ziara
yake hiyo ya kwanza tangu alipoteuliwa kuiongoza wizara hiyo,
alitembelea Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA), pamoja na
kukagua nyumba za Makazi ya Polisi za sasa na zamani zilizopo barabara
ya Kilwa. Wanne kushoto waliokaa ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak
Abdulwakil.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati)
akitoka kuikagua moja ya nyumba ya zamani ya Jeshi ya Polisi ambayo
inakaliwa na baadhi ya askari iliyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Waziri
Kitwanga alizikagua nyumba hizo za zamani pamoja na zakisasa zilizopo
katika eneo hilo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia)
akiiangalia nyumba ya mabati ya makazi ya Polisi wakati alipoingia ndani
huku akitokwa na jasho kutokana na joto kali ndani ya nyumba hiyo.
Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kutembelea nyumba hizo zilizopo
barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishna wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, na kushoto ni mkazi wa
nyumba hiyo, ambaye ni askari Polisi, Nelson Chale.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati)
akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kushoto)
wakizikagua nyumba za kisasa ambazo ni za ghorofa za Jeshi ya Polisi
nchini zilizopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Waziri Kitwanga
alifanya ziara kuzitembelea nyumba hizo ili kujionea ukosefu wa nyumba
unaowakabili Polisi nchini.