Aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la
Ubungo (CCM), Dk. Didas Masaburi jana ameifuta kesi ya uchaguzi ya
kupinga ushindi wa Mbunge, Saed Kubenea.
Maombi ya kufutwa kwa kesi hiyo yaliwasilishwa mahakamani hapo
na wakili wake Clement Kihoko ambapo mahakama hiyo chini ya Jaji Lugano
Mwandambo ilimwamuru Masaburi kulipa nusu ya gharama za kesi kwa
mlalamikiwa( Kubenea)