
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt. Donan Mmbando akieleza kuhusu Mpango wa Taifa wa kudhibiti
magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya Waandishi wa Habari leo
17 Desemba, 2015.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt. Donan Mmbando akionyesha aina ya dawa zinazotakiwa kugawiwa
kwa umma wakati alipotangaza Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa
yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya Waandishi wa Habari leo 17
Desemba, 2015.
Serikali kupitia Mpango wa wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa
yasiyopewa kipaumbele leo imetangaza tarehe 19 hadi 23 mwezi huu kuwa
itaanza zoezi la kugawa dawa kwa makundi yanayopaswa kupata dawa za
magojwa hayo.
Tamko
hilo limetolewa na Katibu mkuu wa Wizara Ya Afya na Ustawi wa
Jamii,Wazee,na Watoto Bw. Donald Mmbando alipokuwa anazungumza na
waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kusema kuwa
Magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele ni Usubi,Vikope (Trakoma),
Matende, Mabusha,Ngiri maji, na Minyoo ya tumbo hivyo dawa hizo
zitasaidia kupunguza tatizo.
Ameongeza
kuwa zoezi hilo la ugawaji wa dawa litatekelezwa katika vituo vyote vya
Afya, Zahanati,Hospitali, shule za msingi na sekondari,sokoni,vituo vya
usafiri,pamoja na Ofisi za Serikali na Mashirika ya Umma na hivyo
wananchi wanaombwa kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo ambayo haina
malipo yoyote.
Katibu
Mkuu huyo amesema kuwa wahusika wakuu katika kupatiwa dawa hizo ni
Watu wote kuanzia miaka mitano na kuendelea,isipokuwa watoto chini ya
miaka mitano,wajawazito, mama anaenyonyesha mtoto chini ya siku saba
na Wagonjwa Mahututi.
“Tunataka kulinda afya zao na Uhai wao hivyo tunaomba wafuate maelekezo vizuri”.Alisema Bw Mmbando.
Aidha
zoezi hilo litatekelezwa katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Singida,
Dodoma,Mtwara, Lindi na Pwani kwa ajili ya kujikinga na kutibu
magonjwa hayo na Mikoa mingine iliyobaki itafanya zoezi hilo katika
ngazi ya jamii na shuleni mwishoni mwa mwezi Januari kuendelea hadi
Februari 2016.
Naye
Mratibu wa Mpango huo Dkt Edward kirumbi ameeleza kuwa takwimu
zainaonyesha kuwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele hapa nchini ni kubwa
ambapo ugonjwa wa Usubi umeenea zaidi katika mikoa sita ikiongozwa na
Dodoma, Ugonjwa wa Minyoo ya tumbo wagonjwa million 13, kichocho
,Matende na Mabusha tathmini za awali zinaonyesha mikoa 18 imeathirika
kwa kuwa na wagonjwa million 12.
Vile
vile Dkt Kirumbi ameeleza kuwa Magonjwa haya yamekuwa na athari kubwa
hasa kwa kuathiri nguvu kazi ya Taifa hivyo wananchi wanapaswa kupata
dawa hizo ambazo zitakuwa zinatelewa kwa mwaka mara moja ili kukinga
upungufu wa Damu, kuuwa vimelea vya ugonjwa huo, kupungua kwa magonjwa
ya ngozi, na kuongeza virutubisho bora mwilini.
Hata
hivyo jamii inapaswa kupewa elimu zaidi kuhusu Magonjwa haya kwa vile
bado haijaelewa athari za magonjwa haya kwa kiasi kikubwa hasa kwa
maeneo ya vijijini ambayo ndio waathirika wakubwa.