Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakiwa wamebeba mfano
wa majeruhi wa ajali, mara baada ya kumuokoa kutoka eneo la tukio wakati
wa maonesho ya kufunga mafunzo ya kozi ya awali ya Sajini na Askari wa
Jeshi hilo yaliyofanyika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakionesha jinsi ya
kuzima moto wakati wa maonesho ya kufunga mafunzo ya kozi ya awali ya
Sajini na Askari wa Jeshi hilo yaliyofanyika Chuo cha Uongozi JKT
Kimbiji jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wakionesha mafunzo ya karate waliyoyapata mara baada ya
kuhitimu kozi ya awali ya Sajini na Askari wakati wa kufunga mafunzo
hayo katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji jijini Dar es Salaam.