Thomas Muller
Kikosi bora cha wachezaji kumi na
mmoja kilichocheza hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya
kimetangazwa na Uefa jambo la kushangaza likiwa kuachwa nje kwa nyota wa
Barcelona Lionnel Messi, Neymar na Luis Suarez.
Washambuliaji
Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Hulk (Zenit St Petersburg) pamoja na
Thomas Muller (Bayern Munich) ndio wanaoongoza safu ya ushambuliaji,
kikosi hicho kikitumia mfumo wa 4-3-3.
Ligi Kuu ya Uingereza imetoa wachezaji wawili, sawa na ligi ya Ujerumani na ile ya Ufaransa.
Suarez messi na Neymar
Mabingwa watetezi wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Barcelona, hawajatoa
hata mchezaji moja katika kikosi hicho licha ya kuwa na safu kiwembe ya
ushambuliaji.
Kikosi kamili ni:
Kipa: Kevin Trapp (Paris Saint-Germain
Mabeki:
Andrea Barzagli (Juventus),Thiago Silva (Paris Saint-Germain), Diego
Godin (Atletico Madrid), David Alaba (Bayern Munich)
Viungo wa Kati: Sven Kums (Gent), Willian (Chelsea), Raheem Sterling (Manchester City)
Washambuliaji: Thomas Muller (Bayern Munich), Hulk (Zenit St Petersburg), Cristiano Ronaldo (Real Madrid).