Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimkaribisha Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ikulu jijini Dar es Salaam na kufanya
Mazungumzo kuhusu hali ya kisiasa ya Zanzibar. Katika Mazungumzo hayo
viongozi wote wamefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ikulu jijini Dar es Salaam.Rais
amemshukuru Maalim Seif na amemsihi waendelee na mazungumzo hadi
suluhisho la muufaka lipatikane.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ikulu jijini Dar es Salaam, wakwanza
kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia
Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika picha na Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.