HAPA KAZI TU; ya Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli
ikiendelea kufanyiwa kazi kama Rais huyo aonekanavyo pichani akiwa
sambamba na mkewe Mama Janeth Magufuli,wakishiriki kufanya usafi leo
ndani na nje viunga vya Ikulu ikiwemo pia soko la Samaki Feri,ambako
alipata wasaa kuwasikiliza wachuuzi wa samaki na wavuvi.
HAPA KAZI TUUU...!!
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiokota
taka taka katika eneo la ufukwe wa ferry akiwa sambamba na mkewe Mama Janeth Magufuli jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (mzee wa hapa kazi tu) akishiriki kufanya usafi na baadhi ya wananchi leo asubuhi katika ufukwe wa ferry jijini Dar Es Salaam.
Rais Magufuli akiendelea kupiga kazi.
Mh, Rais Dkt, John Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiendelea kufanya usafi.
Baada ya kumaliza kufanya usafi, Mh, Rais Magufuli pichani akizungumza na baadhi ya wananchi na waandishi wa habari.