Headlines za soka bado zinachukua nafasi
kila kukicha na mimi siachi kukujuza kila linalonifikia,
hususani katika kuelekea kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili la
mwezi January. Naomba nikusogezee TOP 5 stori za soka zilizoandikwa sana barani Ulaya.
5- Chelsea kutangaza dau la kumsajili Stones mwezi Janury
Baada ya kumkosa John Stones katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August, Chelsea wanapanga kutuma ofa ya pound milioni 40 mwezi January ili Everton wamuachie.
Uamuzi huo unakuja baada ya Terry kuonesha uwezo mdogo dhidi ya mshambuliaji wa Leicester Riyad Mahrez.
4- Man United kumsajili Lukaku mwezi January
Man United wakiwa wanahangaika kupata magoli kutokana na safu yao ya ushambuliaji kutajwa kutokuwa sawa, hivyo wanataka kumsajili Romelu Lukaku ili kuboresha safu yao ya ushambuliaji, stori kutoka ItaSportPress.
3- Van Gaal kumuita Wilson
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal anajiandaa kutaka kuongeza nguvu kwa kumuita kikosini mshambuliaji wake aliyekuwa kwa mkopo katika klabu ya Brighton James Wilson.
2- Monreal kujiunga na Bilbao
Inaripotiwa kuwa kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Aresne Wenger amemuambia beki wa kushoto wa klabu hiyo Nacho Monreal (29) kuwa ruhusa kujiunga na klabu ya Bilbao inayoshiriki Ligi Kuu Hispania Laliga. Beki huyo alikuwa akihusishwa kujiunga na Athletic Bilbao muda mrefu ila kwa sasa mpango huo unatajwa kuwa tayari.
1- Real Madrid wapo tayari kubadilishana na Chelsea Rodriguez na Hazard.
Inaripotiwa na Do Balon kuwa Real Madrid wapo tayari kumuachia kiungo wao mshambuliaji James Rodriguez aondoke Santiago Bernabeu ila kama Chelsea watakubali kubadilishana na Eden Hazard.