Mbunge wa jimbo la Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea amefikishwa
mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam mapema hii leo akielekea katika
chumba cha kusomewa shtaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa Wilaya
ya Kinondoni, Paul Makonda.
Mbunge wa jimbo la Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea akiwa na wanachama
wa chama cha Demokrasia na Maendeleo, leo mara baada ya kusomewa shitaka
lililokuwa likimkabiri katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam
leo.
Mbunge wa jimbo Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea akizungumza na
waandishi wa habari katika mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, Kubenea amekana kufanya kitendo hicho na kesi yake imeahirishwa hadi Desema 29, mwaka huu.