Mawakili wa upande wa serikali na walalamikaji wakiandaa nakala zao kabla ya madai hayo kusikilizwa.
Wakazi wa Kinondoni wakipongezana baada ya kupokea taarifa za kusitishwa kwa bomoabomoa kwenye makazi yao.
Askari wakiimarisha usalama
MAHAKAMA
ya Ardhi jijini Dar imesimamisha zoezi la bomoabomoa iliyowakumba wakazi
maeneo ya mabondeni wa Wilaya ya Kinondoni baada ya wakazi hao
kufikisha ombi hilo mahakamani hapo mapema wiki iliyopita.
Ombi hilo
lilitokana na malalamiko ya wakazi wengi walioiomba mahakama izuie
bomoabomoa hiyo kutokana na madai ya ukiukwaji wa haki zao ambapo wengi
wa walalamikaji hao walidai kufidiwa kabla ya kuondoka.
Hata
hivyo uamuzi huo wa mahakama umewagusa walalamikaji 674 tu ambao
wametajwa kwenye malalamiko huku zoezi la bomoabomoa likiendelea kama
kawaida kwa nyumba zingine ambazo hazihusiki na kesi hiyo.