Gabo Zigamba mwigizaji wa filamu
UNAPOSIKIA
jina la Gabo Zigamba si jina geni katika tasnia ya filamu , Gabo
amejizolea umaarufu katika tasnia ya filamu baada ya kufanya vizuri na
kuwachanganya wapenzi wa filamu Bongo, wengi wakiamini kuwa ni kijana wa
Kimachinga kutoka Kusini kumbe ni Mdigo na Mhehe.
Jina
halisi la msanii huyu ni Salim Ahmed Issa akisema hilo ni jina la
kliniki, lakini jina la riziki anajulikana kama Gabo Zigamba, amezaliwa
Mitaa ya Mshindo na kukulia katika mitaa ya Kitanzini kama ingekuwa hapa
Dar ni mtoto aliyezaliwa Ilala na kukulia mitaa ya Kariakoo akilelewa
na mama yake Rafia Issa Kiyeyeu.
Babu yake
ni Mtogapaafwe Kiyeyeu familia ya Martin Kiyeyeu mtu maarufu sana
Iringa ambaye kila unapotaja jina lake wengi ukumbuka kuhusu maajabu ya
kaburi lake, Gabo anasema kuwa ameishii pande zote mbili lakini sehemu
kubwa sana ni Iringa kwa mama yake akisoma Ipogolo Iringa.
Gabo anasema yeye ni mwanaharakati sauti ya wanyonge isiyosikika hivyo alianza harakati zake kitambo akifiria ni jinsi anavyoweza
kufikisha ujumbe kwa jamii husika kwa kupitia sanaa na hasa filamu,
wengi wanaamini kuwa sinema yake ya kwanza ni Bado Natafuta lakini ni
kazi ilifanya vizuri baada ya kupewa nafasi.
SANAA ALIANZA LINI
Gabo
kuigiza alianza kitambo lakini rasmi ilikuwa ni 2006 kwa kushiriki
katika vikundi mbalimbali huku akiwa na shauku kubwa ya kuwa nyota na
kufikia lengo lake la kuwatetea wasio na nafasi anasema haikuwa rahisi
sana kwani kulikuwa na changamoto nyingi ambazo hazikumkatisha tamaa.
Harakati
zangu hazikuja kama upepo sinema yangu ya kwanza ilikuwa ni Olopong
iliyotengenezwa na Al Riyamy Production chini ya Khalfan Abdalah, hapo
milango ndio ilifunguka kwani baada ya hapo nikacheza 007 Boyz,”anasema
Gabo.
Baada
hapo alishiriki katika filamu ya The Plan, na kujiunga na kampuni ya
marehemu Juma Kilowoka ‘Sajuki’ Wajey Film akishiriki katika sinema zao
kama mwigizaji na kufanikiwa kucheza filamu Mchanga na Keni, The killer
na 007 Days alikuwepo hapo akijifunza vitu katika tasnia ya filamu.
Gabo akiwa na Irene Uwoya, Chopa, Chuchu Hans, Richie katika filamu ya Safari.
Filamu
nyingine alizoshiriki ni Majanga, Safari, Fikra zangu ya Jerusalem Film
ya Jb hizi zote zikiwa za watayarishaji wengine tofauti na filamu yake
ya Kona ambayo aliitayarisha mwenyewe, na sasa amekuja na filamu yake ya
Safari ya Gwalu inayoelimisha jamii ikiwa imetayarishwa na yeye.
Mtayarishaji Vipindi na Mtangazaji
Gabo
ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Bondeni kipindi
kinachorushwa katika televisheni ya Taifa ya TBC1 ambacho kinafuatilia
maisha ya ughaibuni, na kimekuwa kivutio sana kwa watazamaji
wakishuhudia maisha magumu ya ugenini hasa wale walioenda bila mipango
thabiti.
“Kama
nilivyosema awali kuwa mimi ni sauti ya wanyonge wasiosikika nikaona
filamu tu haitoshi kupaisha sauti za wanyonge chini ya menejimenti yangu
tukaja na kipindi cha Bondeni,”
Gabo
ameshatengeneza vipindi vingi sana katika nchi za Afrika ya Kusini,
Zambia, Botswana, Uganda na Malawi na hivi karibuni anatarajia kwenda
nchini Oman kwani kuna watanzania wengi ambao wanapata shida kwa sababu
ya uvivu wa kutofanya kazi.
“Safari
zangu za kurekodi kipindi cha Bondeni imekuwa ikipata ushirikiano na
balozi za Tanzania kwani wao ndio wanatuelekeza sehemu wanazopatikana
watanzania, kwa mfano Oman tumeambiwa watanzania wamekwama na sababu
kubwa hawataki kufanya kazi,”
“Baadhi
ya watanzania wamekuwa wakikimbilia maisha ya ughaibuni huku ni wavivu
wa kujishughulisha, Balozi mmoja ametueleza sisi tunaweza hata kumtukana
bosi kwa sababu ya uvivu wetu,”
Tuzo
Ili
huweze kuonyesha ubora wako na umahiri katika fani yoyote ni pale
unapokumbukwa na taasisi au chombo chochote kwa kutambua mchango wako
katika kile unachofanya, Gabo ana tuzo mbili moja ni Mwigizaji wa bora
wa kiume kupitia tuzo za Action & Cut Views Choice Awards 2014/2015.
Pia mwaka
huu aliweza kujishindia tuzo nyingine kutoka nchini Kenya kwa kupitia
sinema aliyoshiriki ya Queen Masai akiwa kama mwigizaji bora tena wa
kiume.
Changamoto
Gabo
anasema kuwa amekutana na changamoto nyingi lakini yeye kwake ilikuwa
ni chachu ya mafanikio kwani kwani baada ya kushiriki filamu za
watayarishaji wengine aliamua kusambaza kazi zake mlango kwa mlango
kupitia Sarafu Media kutokana na mizengwe ya wasambazaji.
“Sitaki
kujiita jeshi la mtu mmoja kwa ni alama ya mtu kajiita mimi ni hazina
yenye madini joto, wakati tunaanaza kusambaza filamu ya Safari ya Gwalu
vikwazo vilikuwa vingi hadi nikaamua kuzunguka na timu yangu kila
wilaya,” anasema Gabo.
Changamoto
nyingine ni wakati wakati wa kutengeneza vipindi kusafiri kwa muda
mfupi na kufanya kitu ambacho kinakuwa bora lakini kuna wakati
watakutana na watanzania wamechoka wanahitaji msaada wa kurudi Bongo tu
lakini hawana nauli wakihitaji msaada kwake.
Faida
Gabo
anasema moja ya faida kubwa kwake ni pamoja na kupata marafiki wengi
kutoka sehemu mbalimbali lakini faida kubwa kabisa ni kuwa balozi maji
ambayo yatazinduliwa hivi karibuni kiwanda ambacho kitajengwa na
Mtanzania anayeishi Malawi Bishop Simama mfanyabiashara mkubwa sana
nchini Malawi.
Katika
kuenzi ukoo wa mama yake yaani akina Kiyeyeu Gabo amepanga kutengeneza
filamu kubwa ya kufungia mwaka huu itakayojulikana kama Nyumba niitu
sehemu maarufu kwa kuabudia Wahehe kama zawadi kwa babu zake akina
Kiyeyeu na kuimarisha mila na Tamaduni za Babu zake.
Huyu ni Gabo Zigamba maarufu kama Chinga huku akisema yeye ni Chotara wa Kihehe na Kidigo tena wale wadigo wa Mombasa Kisauni.