Mambo si mazuri kwa Mbeya City ambayo imeangushwa kwa kutwangwa mabao 4-1 na wenyeji wake Ndanda FC.
Ndanda FC iliyokuwa nyumbani Nangwanda Sijaona imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao hayo katika mechi ya Ligi Kuu Bara.
Ndanda
FC iliyoitoa jasho Yanga katika mechi iliyopita licha ya kupoteza kwa
bao 1-0, leo ilionyesha soka safi na la kuvutia na kuonyesha kuwazidi
wageni wake katika kila idara.
Wakati Mbeya City ikiangukia pua, Azam FC imefanikiwa kuwaangusha Mgambo FC wakiwa kwao kwenye Uwanja wa Mkwakwaji mjini Tanga.
Mechi hiyo ilikuwa ngumu na yenye kasi licha ya kuchezwa kwenye Uwanja mbovu kabisa wa Mkwakwani.
Stand
United ikiwa nyumbani Kambarage katika mji wa madini mengi zaidi nchini
wa Shinyanga imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya jirani
zao, Toto African.
MATOKEO:
Simba 2-0 JKT Ruvu
Mgambo 1-2 Azam
Ndanda FC 4-1 Mbeya City
Stand United 2-1 Toto
Prisons 2-1 Coastal