Viongozi mbalimbali wa dini wakiwa katika
picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo
(wa pili kushoto walioshikilia bendera), katika Maombi ya Kumuombea Rais
Magufuli na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Maombi
hayo yalifanyika katika Uwanja wa Furahisha Manispaa ya Ilemela Mkoani
Mwanza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa
Serikali na Dini huku pia wananchi wakijumuika pamoja na waumini wa dini
mbalimbali katika maombi hayo.
Mgeni
Rasmi katika maombi hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo
ambae katika hotuba yake, aliwasihi Watanzania wote kuendelea kuliombea
Taifa ili kuondokana na vikwazo mbalimbali ambapo alidokeza kuwa kupitia
maombi kama yaliyofanyika jana, migogoro mbalimbali ikiwemo ya kisiasa
kama iliyopo Zanzibar itamalizika.
Viongozi
mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza
Askofu Charles Sekelwa, Makamu wake Zenobius Issaya pamoja na Kiongozi
wa Kundi la Maaskofu kutoka Jijini Dar es salaam la Good News For all
Ministry Askofu Dr.Charles Gadi pamoja na viongozi wengine wa dini
kutoka mikoa mbalimbali nchini waliliombea Taifa na kuhimiza utuliza
nchini.
Wasaidizi
wa wa Rais Maguguli ambao ni pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu,
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu Mhe.Othman Chande, Spika wa
Bunge Mhe.Job Ndugai, Mawaziri pamoja na viongozi wengine wa Serikali wa
awamu ya tano waliombewa ili kuliongoza vema taifa kwa kuendana na kasi
ya Rais Magufuli.
Viongozi mbalimbali wa dini wakiwa katika
picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo
(Wa tatu kushoto) katika Maombi ya Kumuombea Rais Magufuli na Taifa
yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.