Mradi wa
Kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia Tasinia ya Urembo ujulikanao kama
Manjano Dream Makers hatimaye umefika Mwanza.Wataalamu wa Maswala ya
biashara na Urembo Wataendesha Mafunzo Wiki ijayo Traehe 18.01.2016
Kwenye Ukumbi wa Rock city Mall Jijini Mwanza,Wanawake 35 wa jiji la
Mwanza Watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi vya
LuvTouch Manjano.
Wanawake
Wakazi wa jiji la Mwanza Mwanza Wanaopenda Kunufaika na Mradi huo
Wanaombwa Kujitokeza Kwa wingi Kujiandikisha siku ya Kesho Tarehe
15.01.2016 kuanzia saa Mbili Asb kwenye Ukumbi wa Rock City Mall .
Mafunzo
yana Lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua. Awamu ya
kwanza ni kumfundisha maswala ya Biashara namna ya kuibua na kubuni
miradi mbalimbali namna ya kuandika Mpangilio wa Biashara ikiwemo
Matumizi sahihi ya Rasilimali Muda, Fedha, Muda na pia namna ya
kujitunzia akiba itokanayo na Biashara yake.
Baada ya
Wanawake hawa kuhitimu Mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa
Mikopo kwajili ya kuwawezesha Kuanzisha Biashara wakiwa chini ya
Uangalizi Maalum wa taasisi hiyo kwa Lengo la Kuhakikisha kila Mhitimu
wa Mafunzo haya anapiga hatua na kuweza Kujitegemea.