Hospitali
ya Taifa Muhimbili imesema kuwa inaendelea kuboresha huduma za afya ili
kupunguza msongamano wa wagonjwa kupitia utaratibu mpya wa madaktari
Bingwa kuwaona wagonjwa kupitia Kliniki zilizoanzishwa katika hospitali
hiyo.
Mkuu wa
Idara ya Huduma ya Wagonjwa wa Nje wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Dkt. Raymond Mwenesano akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam amesema kuwa
utaratibu huo utawasaidia wagonjwa kupata huduma kwa wakati na kupunguza
muda kusubiri huduma.
Amesema
utaratibu huo utawahusu wagonjwa wote wanakwenda kutibiwa katika
Hospitali ya Muhimbili na kuondoka hususan wale wanaolipa fedha taslimu
na wale ambao ni wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bima za
mbalimbali za Afya na watumishi ambao makampuni yao yana mikataba na
Hospitali kutibu wafanyakazi wao.
Dkt.
Mwenesano ameeleza kuwa tayari Kliniki hizo zimekwisha anza kufanya kazi
na kuongeza kuwa katika hatua hiyo madaktari Bingwa pekee ndiyo
watakaoona wagonjwa wakati wa siku za kazi kuanzia saa 3 asubuhi mpaka
saa 12 jioni, pia jumamosi kuanzia saa 3 asubuhi hadi za 8 mchana.
“
Muhimbili tumeamua kufanya mabadiliko haya kuanzisha Kliniki na
kuwatumia madaktari bingwa peke kwa lengo la kuboresha huduma zetu,
awali tulikuwa na Kliniki hizi lakini huduma zake zilikuwa hazitolewi
kwa kiwango cha kuridhisha kutokana na kutokuwepo kwa muda wa kutosha wa
mdaktari hao kuhudumia wagonjwa” Amesisitiza.
Aidha,
amefafanua kuwa wagonjwa wanaopatiwa rufaa kuja hospitali ya Muhimbili
wataendelea na utaratibu wa kawaida wa kwenda na Barua za Rufaa ili
waweze kupatiwa huduma.