Bingwa wa
michezo ya Riadha ya walemavu Oscar Pistorius, ambaye alimuua kwa
risasi mpenzi wake mwaka 2013, ameiandikia rasmi Mahakama ya Katiba,
Mahakama ya juu ya nchini Afrika Kusini, kupinga hukumu dhidi yake.
Pistorius alipatikana na kosa la mauaji baada ya upande wa mashataka kukata rufaa.
Mwanasheria
wa mwanariadha huyo mlemavu, Andrew Fawcett amethibitisha barua hiyo ya
mteja wake, akibaini kwamba ana imani kuwa mahakama ya Katiba itachukua
uamzi wa kuridhisha kwa mteja wake
"Tumewasilisha
maombi kwa ajili ya rufaa kwa Mahakama ya Katiba", Andrew Fawcett,
mmoja wa wanasheria wa mwanariadha wa zamani, ameliambia shirika la
habari la Ufaransa AFP.
Wakati wa
kesi yake katika Mahakama ya mwanzo, Pistorius, aliokatwa miguu miguu
miwili, alipatikana na kosa la mauaji bila kukusudia na kuhukumiwa
kifungo cha miaka mitano jela mwaka 2014.
Lakini
Mahakama Kuu ya Rufaa ilirejelea hukumu hiyo na kubaini, Desemba 2015,
kwamba Pistorius alihusika na "mauaji". Kwa sasa Pistorius anakabiliwa
na adhabu ya kifungo cha miaka 15 jela. Hukumu yake bado haijatolewa.