Kweli
wachezaji wakikutana wakati mwingine wanakuwa utafikiri watoto; mfano
mzuri ni Cristiano Ronaldo aliyeamua kumfinya sikio beki Sergio Ramos
wakati wakipiga picha maalum wakiwa na Rais wa Real Madrid, Florentino
Perez.
Perez
alikuwa akipiga picha na vijana wake, Ramos alikuwa karibu kabisa
akizungumza na milionea huyo. Haraka Ronaldo akamfinya sikio Ramos
anayejulikana kwa ukorofi.
Kwa
kuwa alikuwa akizungumza na Rais wa klabu, akashindwa hata kugeuka na
kujikuta akivumilia alichokuwa akifanyiwa na mshikaji wake.