Saud
Arabia imesitisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi ya Iran na huku
kukiwa na hali mbaya ya mvutano kufuatia utekelezaji adhabu ya kifo kwa
mhubiri maarufu wa dini ya kiislamu kutoka mjini Riyadh .
Waziri wa
mambo ya kigeni wa Saud, Adel al-Jubeir, ameishutumu serikali ya Iran
kwa kusambaza silaha na kuanzisha jela na kuwafunga watu wanaodhaniwa
magaidi katika ukanda wake .
Waziri
huyo ameongeza kusema kwamba ,wana diplomasia wa Iran wametakiwa
kuondoka Saudia ndani ya saa arobaini.Mwishoni mwa wiki iliyopita,
waandamanaji mjini Tehran waliuvamia ubalozi wa Saudi ,huku wakilaani
utekelezaji wa hukumu ya kifo kwa Sheikh NIMR al-NIMR na watu wengine
arobaini na sita.
Watu hao
waliouawa inasadikiwa walikuwa na hatia ya makosa yanayohusiana na
ugaidi.kiongozi mkuu wa Iran alimuelezea Sheikh huyo kama shahidi ambaye
alikuwa akitetea amani na kufanya maandamano ya amani.BBC