Picha
Rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli itaanza kuuzwa Januari 08, 2015, katika Ofisi za
Idara ya Habari (MAELEZO) Mtaa wa Samora.
Kila
nakala ya picha hiyo itauzwa shilingi Elfu Kumi na Tano tu bila fremu.
Picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere itauzwa shilingi Elfu Tano
tu. Aidha, Picha hizo zitauzwa katika Ofisi za Wakala wa Huduma ya
Ununuzi Serikalini (GPSA).
Picha
hizo zinatakiwa kutundikwa katika ofisi zote za Serikali, Taasisi za
Umma, Mashirika na Ofisi binafsi. Kila ofisi inatakiwa iwe na picha ya
Mhe. Rais pamoja na Baba wa Taifa.
Serikali
inatoa onyo kwa wale wote wanaosambaza picha isiyo rasmi pamoja na
Serikali kutoa taarifa kusitisha matumizi ya picha hiyo na
wanaotengeneza picha ukubwa ambao siyo rasmi.
Hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Idara ya Habari(MAELEZO) ndio yenye Haki miliki ya picha hiyo.