Utafiti uliofanywa nchini Kenya
umeonyesha kuwa wanaume wa mikoa ya Magharibi, Nairobi na Nyanza
wanaongoza kwa kukabiliwa na vitendo vya kunyanyaswa, kudhalilishwa
na kupigwa na wake zao.
Utafiti huo ambao ulikuwa ukijaribu
kupigana na mtazamo kuwa wanaume wa mkoa wa Kati Kenya wanakabiliwa
zaidi na vitendo vya ukatili na vipigo kutoka kwa wanawake wao,
umebaini nusu ya wanaume waliohojiwa katika mikoa hiyo wamepata
vipigo, kudhalilishwa kingono na kuthiriwa hisia zao na wake zao.
Matokeo ya utafiti huo yametolewa
jana katika uzinduzi wa utafiti wa idadi ya watu na hali ya afya,
uliofanywa mwaka 2014, unaolenga kuangalia idadi ya watu Kenya pamoja
na hali za afya za wananchi.