Matumaini ya mwanamke wa Mombasa
Kenya aliyeolewa na wanaume wawili ya kutaka kutengana na mume wake
wa kwanza ambaye mapenzi yamechuja, yamefanikiwa baada ya mahakama
kuridhia kuvunja ndoa yake hiyo.
Hata hivyo, hukumu ya Mahakama ya
Kadhi imemuagiza mwanamke huyo Rehema Dzuya kurejesha mahari ya
samani za ndani zenye thamani ya shilingi 40,000 za Kenya alizotoa
mumewe kama mahari.
Hata hivyo mume wa Rehema, Salim
Twota amepinga maamuzi hayo ya Mahakama ya Kadhi, kwa madai kuwa
yamempendelea mkewe, na kukesma atakata rufaa katika Mahakama Kuu kwa
kuwa bado anampenda mkewe.
Kadhi Mkuu wa Mombasa Abdulhamin
Athman amevunja ndoa hiyo kwa kusema ni vigumu sana kwa Rehema na
mumewe Salim kuishi pamoja.