Mchezo wa Ligi ya NBA uliochezwa
jana usiku Jijini London Uingereza umehudhuriwa na mastaa mbalimbali
wa soka nchini Uingereza.
Nyota wa Ligi Kuu ya Uingereza wa
sasa na wa zamani walifika kwenye uwanja wa O2 Arena kushuhudia
Toronto Raptors wakichuana na Orlando Magic katika mchezo huwa wa
kila mwaka Jijini London.
Wachezaji wa Arsenal na Chelsea
nimiongoni mwa walioshuhudia mchezo huo wa NBA, huku mshambuliaji wa
zamani wa Chelsea, Didier Drogba akipata fursa ya kuonyesha uwezo
wake katika kikapu pia.
Didier Drogba akionyesha uwezo wake wa kucheza kikapu
Alex Oxlade-Chamberlain, Carl
Jenkinson na Olivier Giroud wakifuatilia mchezo huo wa NBA
Mchezaji wa zamani wa Chelsea
Michael Ballack akifuatilia mchezo huo akiwa na mpenzi wake Natacha
Tannous