HENRIETTE REKER MEYA WA MJI WA COLOGNE
Kansela
wa Ujerumani, Angela Merkel, ameshtushwa na madai kwamba wanawake
wapatao tisini walinyanyaswa kingono wakati wa sherehe za kuukaribisha
mwaka mpya wa 2016 mjini Cologne.
Polisi
pamoja na mashuhuda wa matukio hayo wameelezea mashambulio hayo ya
kingono kuwa yalitekelezwa karibu na eneo maarufu la cathedral, ambalo
lilikuwa limefurika idadi kubwa ya makundi ya wanaume wenye asili na
muonekano wa Ki arab ama Afrika Kaskazini.
Merkel
ametoa agizo la kufanyika uchunguzi wa kugundua ukweli kuhusiana na
madai hayo na kisha kuwaadhibu wahusika ,bila kujali asili yao ama
historia za awali.
Meya wa
mji wa Cologne, Henriette Reker, ameonya juu hatua zitakazochukuliwa
zitende haki bila ya kuwaelemea wakimbizi walioingia nchini Ujerumani.Na
akachukua hatua ya kufanya mazungumzo ya dharula na maafisa wa polisi
kuhusiana na mgogoro huo; ambapo Polisi waliahidi kuimarisha ulinzi.