Rais
wa Nigeria, Muhammadu Buhari, atalazimika kufanyia kazi zake akiwa
nyumbani baada ya panya kuharibu ofisi yake iliyopo Ikulu.
Msemaji
wa Rais Buhari, Garba Shehu, amesema, panya hao wameharibu samani za
viyoyozi katika ofisi hiyo hivyo kiongozi huyo hawezi kufanya kazi
katika ofisi mbovu ambayo itakarabatiwa kwa kipindi cha miezi mitatu.
Bw. Garba amesema, hatua ya Rais Buhari kufanyia kazi zake nyumbani hakutaathiri ufanisi wake kwa aina yoyote ile.
Rais
Buhari alirejea nyumbani Nigeria Jumamosi iliyopita baada ya kukaa
Jijini London nchini Uingereza kwa zaidi ya siku 100 alikokuwa akipatiwa
matibabu kwa ugonjwa ambao hata hivyo haujawekwa wazi.