Raisi
wa Zanzibar ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Muhammed Shein
amewataka mawaziri kuhudhuria Vikao na Ziara zake ili waweze kujua
matatizo yanayowakabili wananchi katika jamii.
Akizungumza
baada ya kupokea Mpango kazi wa utekelezaji wa ilani ya Chama cha
mapinduzi kwa Serikali ya Mkoa wa Mjini Maghari katika ukumbi wa Baraza
la Wawakilishi kikwajuni Mjini Zanzibar,
Dk.
Shein amesema ni wajibu wa kila kiongozi kutekeleza ilani ya CCM hivyo
si vyema kwa baadhi ya mawazi kukwepa kuhudhuria Ziara zinazoendelea
jambo linalowakosesha wananchi haki zao za msingi.
Amesema
ziara Zinazoendele katika mkoa huo imekusudia kuangalia miradi
mbalimbali ya maendeleo ambayo inatekelezwa na serikali kupitia ilani
ya Chama cha Mapinduzi CCM, ili kuhakikisha wananchi wananufaika na
miradi hiyo katika jamii pamoja na kuimarisha amendeleo katika Nchi.
Wakati
huo huo Dk. Shein amefungua Tawi la CCM Muembe Matarumbeta na kuwataka
Viongozi wa tawi hilo kulitumia tawi kwa kukiendeleza chama pamoja na
kuwa watekelezaji wa ahadi za wananchi katika kuleta chachu ya maendeleo
katika jamii.