Wakili maarufu nchini Peter Kibatala amewasili katika jiji la Mbeya ili kuwawakilisha Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za juu Kusini, Emmanuel Masonga.
Sugu na Masonga wanakabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli ambayo wanadaiwa kuitoa December 30, 2017 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge.
Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea leo kwa Sugu na Masonga kuanza kutoa utetezi wao chini ya wakili wao mpya Kibatala baada ya mawakili wao wa awali, Boniface Mwakubusi, Sabina Yongo na Hekima Mwasipu kujitoa katika kesi hiyo.