Mh. Godbless Lema
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema azungumzia kifo cha Kada wa Chadema Tambwe Hizza
Mh. Lema amesema kuwa utu na haki ndio kifo halisi katika maisha yetu na kuandika maneno haya katika ukurasa wake wa twiter kuwa “Watu wengi wanafikiri kufa ni jambo baya na gumu,lakini ukweli ni kwamba kuishi bila wajibu,utu na haki ndio kifo halisi katika maisha yetu,wewe Tambwe uliishinda hofu .Utaendelea kuishi,” ameandika Lema kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Marehemu Tambwe Hizza amefariki akiwa ni mmoja wa waratibu wa kampeni za chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) katika jimbo la Kinondoni.
MAREHEMU TAMBWE HIZA
Tambwe Hizza amefariki Dunia leo alfajiri nyumbani kwake Mbagala Kizuiani, jijini Dar es salaam.
Inaelezwa kuwa Marehemu Tambwe Hizza amefikwa na mauti hayo akiwa usingizini, kwani jana mpaka usiku alionekana kuwa mzima na hana dalili zozote za kuumwa.
Taarifa za msiba huu zimethibitishwa na Msemaji wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tumaini Makene.
Msiba upo nyumbani kwa marehemu, Hizza huko Mbagala Kizuiani, Jijini Dar es salaam.
Mungu ailaze mahapa pema roho ya Marehemu Tambwe Hizza - Amen.