HUYU NDIE WA UKWELI UKWELI BABU EEEEH! SHAURILO.
Huyu ndiye Munawar khamis a.k.a Munaiz wa ukweli ukweli, mtoto kaenda hewani kama twiga mama wa kipindi cha sasambu sasambu na mahaba ya dhati ndani ya radio ya 90.9 chuchu fm. Hapa alikuwa MC katika ukumbi wa magereza hapa zenji kwenye onesho la mambo ya kipwani pwani zaidi katika kunyongesha nyonga na kuzungusha panga boi, he he ya,
Lakini leo pia patakuwa hapatoshi katika ukumbi huo huo wa magereza katika mpambano wa kukata na shoka kati ya vikundi vikali vya miondoko hiyo hapa zenji kati ya JKU na East African Modern Taarab.
Mdau hilo ni bonge la pambano linaloletwa kwako na wataalamu wa burudani hapa Zanzibar wanaitwa Taff Promoshen wakishirikiana na kituo cha Redio cha 90.9 Chuchu fm.
KWA TAARIFA YAKO TU, DON'T MISS IT...!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!