HII ILIKUWA NI KATIKA KUELEKEA KWENYE BESI DEI YA RADIO MAARUFU VISIWANI ZENJI YA 90.9 CHUCHU FM YAANI '' hemkwaa 2008-2009'' .Hapa ilikuwa ni kidongo chekundu ambapo kituo hicho cha redio kiliandaa msosi maalum wa mchana na kujumuika na wagonjwa wa akili hafla iliyofanyika hospitalini hapo.
Jamaa anaitwa Mussa Bonge kutoka chuchu fm akiwapakulia waheshimiwa sana bonge la msosi.
Mshikaji naye hakuwa nyuma, Haji a.k.a mzee wa meza alikuwepo kumpa tafu Mussa bonge, hapa sijui walikuwa wanashauriana kitu gani, msosi uliisha nini?????
Hilo ndio lile tunda la manjano ''yellow fruit'' akiwa plate yake tayari kwa kupata lunch huko kidongo chekundu kushoto yake ni C-9.

Huyu ni mheshimiwa sana a.k.a mjommba wenu kween'h hapa akifuatili kwa makini na kuhakikisha je maagiz aliyowapa vijana wake yanakwenda kama alivyopanga? Bila shaka yalienda sawa bin sawia.

Hapa bosi kibano a.k.a mjomba wenu kween'h akisisitiza jambo fulani,pembeni yake ni Shorty Mwenda au unaweza kumuita bosi mfupi.

Hapa mheshimiwa na nihii akifuatili matangazo ya live a.k.a ya moja kwa moja kutoka katika eneo hilo la tukio hadi studio kuu iliyopo Mlandege.
Mnyamwenga huyo hapo ni mtangazaji wa 90.9 Chuchu fm anaitwa Halifa Mmanga (Ras Midude) mwenye kofia nyeupe aki-show love na baadhi ya wagonjwa hao wa akili.