Mnyamwenga huoy hapo.!!!!!! Mchizi huyo hapo.!!!!!!!!!!

Jamaa ukikutana naye njiani huwezi kuamini kama ndio yule tunayemskia redioni kutokana na sauti yake kamwili kadogo lakini bonge la sauti yeye anaitwa Greygory Henry a.k.a G voice, G mopa, hapa anawajibika katika stesheni ya 90.9 Chuchu fm akiwa anaendesha kipindi chake cha East Africa Fleva a.k.a mofire.

Kutoka kushoto ni watangazaji wa 90.9 chuchu fm Halifa Mmanga(Ras Midude), Issa Ndokeji na Daniel Kijo (Danny Kijo ) wa chanel five wakiwa katika pozi huku wakibaadilishana mawazo . Mdau hebu tujiulize mimi na wewe ni kwa nini vijana wengi siku hizi wanakimbilia katika fani ya uandishi wa habari na utangazaji? ma dada du kibao pamoja na mabraza meni wanakimbilia fani hiyo?
kama huamini hebu fanya uchunguzi utagundua kwamba katika kila vijana kumi basi saba ni waandishi wa habari au watangazaji, tuambiane jamani au wenzetu kazi zenu zinapatikana ki urahisi zaidi nini ? aaah! mimi natania tu mjomba lakini wadau wanataka kufahamu why vijana wengi siku hizi hizi wapo katika fani hiyo?
Kama utakumbuka vizuri enzi za Mwalimu watangangazaji wote walikuwa ni watu wazima, kama vile kina Malima Ndelema, Charles Hillary, Julius Nyaisanga, Salim Mbonde, Ben kiko pamoja na wengine wengi tu, lakini eti siku hizi hata mdogo wangu Yellow fruit naye ni mtangazaji, duh, najuuuuta kuwafahamu!!!!!!!!!!
HAYA VIJANA CHANGAMOTO KWENU HIYOOOOOO..!!!!!!!!!!!!!!!!