
Mwanzoni wa miaka ya themanini mpaka kati kati ya miaka ya tisini muziki wa kikongo maarufu kama bolingo kutoka nchini Kongo ulitesa sana katika tasnia ya muziki hasa katika nchi zetu hizi za ki- Afrika.
Na utakapoizungumzia bolingo hutaacha kuwataja wakali wa muziki huo kama vile; Koffi Olomide' mopao mokonzi, papaa fololo', Le grande Joseph Kabasele Yampanya'pepe kale na kundi lake la L'empire bakuba, Papa Wemba, Wenge Musica, Extra Musica, J'b Mpiana, Madilu System, Kanda Bongoman, Awilo Longomba pamoja na wakali wengine kibao ambao kama nikisema niwaorodheshe basi nitafika kesho.
Mimi nikiwa kama mshika dau wa muziki huo wa kikongo yaani bolingo najiuliza bila kupata jibu je muziki huo umekufa au la! na kama umekufa je umefia wapi? Mapromota wengi wa kipindi hicho kama Kayembe Chez- Ntemba na wengine kibao walijitahidi kwa uwezo wao hata kuwaleta baadhi ya wasanii kutoka nchini kongo kuja kutumwagia maburudani.
Hadi ikafikia wakati nikajiuliza inawezaekena kule kongo kwa sasa hakuna maslahi labda kwa sababu wanamuziki hao hao wa kikongo kama kina Nyoshi El- saadat, Elyston Angai, Mule mule Fbi, na wengine wengi tu wametia timu bongo na kupiga muziki katika bendi kadhaa kama vile Fm Academia, Vibration Sound, Diamond Sound na nyinginezo. wakongo wenyewe wanasema wenyewe wanasema '' TOKOMONA NDELELO"