WATOTO WA MJOMBA WALICHEZEA KICHAPO.
FULL NGWAMBA YA CHUCHU FM
WATOTO WA GHORONI CHUCHU FM WAKIPATA SNEPU YA PAMOJA KABLA YA KUANZA KWA GEMU KATI YAO NA KITUO KULELEA WATOTO YATIMA S.O.S MJINI ZENJI GEMU ILIYOPIGWA KATIKA UWANJA WA HOME WA S.O.S, AMBAPO MA-PRESENTER HAO WA CHUCHU FM WALIGONGWA MAGOLI 4-1.
GEMU HIYO ILIKUWA NI KATIKA MAANDALIZI YA KUTIMIZA MWAKA MMOJA KWA KITUO HICHO CHA MATANGAZO CHA CHUCHU FM RADIO AMBAYO IMEBATIZWA JINA LA ''HEMKWA!!!!''.
AMINI USIAMINI BETHIDEI HIYO ILIFUNIKA MBAYA KWANI ILIKUWA NI YA KIPEKEE ZAIDI, UNUJUA NI NINI! KWANZA SHEREHE ZOTE HIZO ZILIDUMU KWA SIKU NNE MFULULIZO PAMOJA NA KUSINDIKIZWA NA WASANII WAKALI KIBAO KUTOKA NDANI NA NJE YA ZANZIBAR.
HEBU CHEKI LISTI LAO:
Waliosimama kutoka left ni: Zaituni Makwali(yellow fruit), Greygory Henry(G-voice), Dj. Cool Para, Dj. Snake, Khalifa Mmanga (Ras midude), Dj. Lat(bwan' faki), mjomba kweenh!!!!(bosi kibano), Dada Judy.
Waliochuchumaa kutoka left ni: Haji(mzee wa bwaga moyo), Maua, Merry Mwita(white rose), Mussa Mbarouk(bonge),
Mstari wa kwanza mbele: zeudi mvano, Emmanuel Sokone(Master E mzee wa blog), Dj. Ebby,(mzee wa mashantale), Shorty Mwenda(bosi mfupi), Rehema Nyamaka( lady kiss) Wazee wamependeza kinoma na uzi wao wa Barca na bado wakachezea mkongo'oto, jamani soka sio saizi yenu nyie nendeni studio mkazionee mixer maikrofoni na ma-nyumaki.