
PICHANI JUU NI RAIS JK, RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMIN MKAPA, PAMOJA NA WAZIRI WA MAJI MARK MWANDOSYA WAKIENDA KUKAGUA MITAMBO YA KUSAFISHA MAJI ILIYOPO KATIKA KIJIJI CHA IHELELE WILAYA YA MISUNGWI.
MRADI HUO ULIASISIWA NA MH.MKAPA KATIKA KIPINDI CHA UONGOZI WAKE. MRADI HUO MKUBWA WA MAJI KUTOKA KATIKA ZIWA VICTORIA UTAWASAIDIA WATU WA MIJI YA SHINYANGA, KAHAMA NA PENGINE HATA TABORA.

HAPA MH. RAIS JK AKIFUNUA KITAMBAA KWENYE JIWE LA MSINGI KATIKA KITUO HICHO CHA MRADI WA MAJI MJINI KAHAMA NA SHINYANGA AMBAPO RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU MH. BENJAMIN MKAPA ALIHUDHURIA.
KUSHOTO YA JK NI WAZIRI WA MAJI BW. MARK MWANDOSYA.

HUYO NI BI. JANETI FADI MKAZI WA NDALA SHINYANGA AKITWISHWA NDOO YA MAJI NA RAIS JK HII INAASHIRIA KUKAMILIKA KWA ZOEZI ZIMA LA UZINDUZI HUO WA MRADI MKUBWA KABISA WA MAJI NCHINI.
MTOTO FARIDA FADI AKIPONGEZWA NA RAIS JK BAADA YA KUIMBA SHAIRI ZURI KATIKA HAFLA HIYO. MSANII HUYO CHIPUKIZI NI MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI NDALA, SHINYANGA MJINI.