
Jana mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) imeonesha uhai wake baada ya kuzuia safari ya boti ya MV Sepideh Kuondoka katika Bandari ya Dar- Es- Salaam kwenda Zanzibar na Pemba kutokana na boti hiyo kujaza abiria zaidi kupita kiasi.
MV Sepideh ambayo kisheri inatakiwa kuchukua abiria 250 lakini yenyewe ilizidisha idadi hiyo kwa kuchukua abiria 325.
Blogu hii ya AMANI NA UPENDO inatoa pongezi kwa (SUMATRA) kwa kuliona hilo na kulifanyia kazi mapema kwani wahenga wanasema 'kinga ni bora kuliko tiba' na pia zoezi lenu hilo lisiishie hapo.
JAMANI WAMILIKI WA VYOMBO HIVYO VYA USAFIRI MSITUFANYIE HIVYO MTATUMALIZA..!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!