Mwanamuziki maarufu kutoka jamhuri ya kidemokrasia ya kongo ambaye pia ni balozi wa THE MULTLATERAL INITIATIVE ON MALARIA(M.I.M) Koffi Charles Antoinne Olomide papa fololo quadra ma pia waweza kumuita mopao sarkozii yupo nchini kwa ziara ya siku mbili, ambayo ni hisani kutoka shirika la umoja wa kimataifa la kuhudumia watoto duniani(UNICEF).
Mbali na hayo lakini pia papa fololo atapata nafasi ya kuzuru mji wa kihistoria wa bagamoyo kabla ya kumalizika kwa ziara yake hiyo.
Olomide mbali na mafaaniko ambayo ameyapata lakini pia na mwanamuziki anayeaminika kuwa na maringo kwa sana tu.
Na inasemekana kwamba mopao amekuwa kivutio kwa wapenzi wake hasa kwa kunyuka pamba za ukweli.

Pichani juu Mopao akidondoka winoa .k.a akisaini, mara baada ya kukanyaga ardhi ya bongo.
Hapa sijui mtu mzima ameombwa aingize voko kwa ajili ya jingo,!!? kushoto yake ni nani hii ambaye ni bosi mkubwa wa kituo cha 88.4 Clouds Fm na kulia ya papa fololo ni Sophia Kessy.

Vipi Sophy niko bien au nimekosea.!!!

Weeeh! uko bien sana monsieur, mimi nakuamia kwa sana tu papa fololo.

Nisaidie mdau, hapa Koffi anaelekezwa jinsi ya kuingiza voko ya jingo, au lugha iliyo tumika kuandika hiyo script yenyewe ndio probleme.

Huyo ni Dj. Too Short anayeaminika kuwa ni mkali wa m wa kuzimix bolingo, aki shoo love na Koffi Olomide.