Jamani haya sasa ni Makubwa.! Siku nyingi tumekuwa tukiona kina kaka na kina baba ndio wapo mstari wa mbele katika 'kushadadia' timu mbali mbali hapa Tanzania pamoja na ulimwenguni kwa ujumla.
Na wamekuwa wakiyaonesha mapenzi yao hayo hadharani kiasi kwamba hata kama ukikutana naye huko kitaani utajua tu huyu ni ni shabiki wa timu fulani kutokana na jezi 'uzi' wa timu aliyoivaa., kama ni Man u, Liverpool, Arsenal, Chelsea, Simba, Yanga au yoyote ile.
Sasa mdau leo asubuhi nimeshangaa nilipoamka na kumkuta wifi yenu amevaa jezi 'UZI' huo anaoonekana nao hapo pichani, lakini nikashindwa kujua ni wa timu gani. Kiukweli ameng'ara mtoto wa kipare lakini wadau wanataka kujua wewe ni shabiki wa timi gani?????? kama wewe ni wa msimbazi, old traford au bwawa la maini. TUWEKE WAZI TUJUE MAMAAAAA....!!!!!!!!!!!!!!