Kituo cha Radio cha Hits Fm kwa ushirikiano Na Zanzibar Cable Television kimekuandalia bonge la shoo ya kukata na mundu, itakayofanyika katika ukumbi wa Gymkhana hapa Zanzibar siku ya jumamosi ya wiki hii ya tareha 9.10.2010.
Kwa mujibu wa mratibu wa Tamasha hilo Shorty Mwenda amewataja wasanii watakaoupamba usiku huo kuwa ni Diammond, Samy na Samir. Mratibu huyo ameongeza kuwa wasani watakaowakilisha kutoka Visiwani hapa ni Berry Black, Rico Single, na Mwana dada Dorica anayetamba na ngoma yake iitwayo Chaguo langu.