JAMANI, hiyo picha ni hospitali. Fikiria, huyo mgonjwa hapo anaondoa maumivu au ndio anazidisha maumivu? Huu ni mwaka (46) tangu nchi hii ikombolewe kutoka mikononi mwa wakoloni lakini hospitali haina vitanda wala chandarua, vilivyopo ni vya kamba na wala havina magodoro chupa za maji 'dreep' zimetundikwa madirishani. Je! tunakwenda mbele au tunarudi nyuma kwa hatua mia moja?
Hii ni shule ya msingi, ambayo inategemewa kuja kutoa marais, wabunge, madaktari, marubani, mabaharia na watu wote muhimu unaowafahamu wewe. Lakini hebu itazame vizuri hiyo shule, halafu jiulize hivi.!? Je! huo mkakati wa kuinua kiwango cha elimu nchini upo au ni 'DANGANYA TOTO?'
Hao ndio hao viongozi wetu wa baadae tunaowasubiri waje kuwa na nyadhifa mbala mbali serikalini na hata katika taasisi binafsi. Je! hapo kuna marubani, marais, wabunge na madaktari kweli? Tumlaumu nani kati ya serikali, wizara ya elimu, mwalimu anayefundisha au wazazi wa watoto hao.
BLOGU HII INAKUOMBA NA KUKUSHAURI KUITUMIA VIZURI NAFASI YAKO YA KUPIGA KURA MWAKA HUU. KWANI TUNAHITAJI VIONGOZI
BORA NA SIO BORA VIONGOZI