Baunsa akihakikisha usalama wa kutosha kwa mwimbaji na pia rapa wa bendi ya mwanamuziki Ferre Golla kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayekwenda kwa jina la (Shikito) Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mwl. Julius Kambarage Nyerere jijini Dar Es Salaam Alhamisi iliyopita na Ijumaa waliuwasha moto wa burudani katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
"Mkali" Shikito ambaye anafanya vizuri na bendi ya Ferre Golla akihojiwa na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa J.k Nyerere jijini Dar Es Salaam. Baada ya Ferre Golla kukata kiu ya wakaazi wa Dar mzigo ukapelekwa kanda ya ziwa jijini Mwanza.