Hebu tujaribu kuuangalia mustakabali wa maisha ya msanii Elizabeth Michael a.k.a 'Lulu'. Amefikia kusema hadharani kwamba eti akivaa nguo ndefu anawashwa.! Na kwa kulithibitisha hilo hebu angalia hiyo nguo aliyoivaa hapo juu pichani. Najaribu kujiuliza je! anawashwa mwili kama alivyosema au kuna mengine? Lakini vipi kwa upande wa wazazi wake pamoja na ndugu zake kwa ujumla, wameichukuliaje tabia hiyo ya mtoto wao?
Haya! tazama tena picha hiyo hapo, bila kujali nani anamtazama, mtoto wa kike 'full' kujiachia na kivazi chake kama yupo ufukweni vile.
Kaka yenu swali langu ni moja tu. Kama kioo cha jamii anafanya hivyo, je! jamii iige nini kutoka kwake? Mdau jibu bakia nalo wewe mwenyewe.