sokonejr.blogspot.com
Tuesday, December 6, 2011
WERRASON NGIAMA MAKANDA.
Mfalme wa msitu ambaye pia ni kiongozi wa kundi la Wenge musica maisom mere (WMMM) Werraso Ngiama Makanda ama 'igweee' akiwa ufaransa kwa show ya international african music festival amekutana na kipigo akiwa katika mgahawa unaomilikiwa na mama wiva huyu ni mke wa Josky Kiambukuta kutoka kwa watu wanaojiita combatants.
Katika mgahawa huo pia watu walioathirika ni wanasiasa ambao hawakutajwa majina yao pamoja na mama wiva na wateja wengine. werrason alijikakamua kuchapana na jamaa mmoja kwani werra aliwahi kupata mafunzo ya juu ya kungfu na kupata tuzo akiwa kijana mdogo,
combatatnts ni genge la wahuni ambao kwasababu zao huwashambulia wanamuziki kadhaa wanaofanya maonyesho ulaya na hasa wenye mashabiki wengi,
hata mashabiki wa wanamuziki hawa huathirika pia na ndio maana hivi karibuni wamekuwa wakihofia kuhudhuria maonyesho kadhaa wakihofu kudhurika. Hali hii imeshusha sana mapato ya wanamuziki wa kongo wanaozitegemea show za ulaya kimapato....
Mbali na hayo yote lakini kwa sasa Werrason yupo hospitali karibu wiki moja sasa akipata matibabu baada ya kupata ajali ya gari iliyosababisha kuvunjika mkono.
POLE SANA IGWEEEEE WASIRUDISHE NYUMA MAANDALIZI YAKO YA ALBUM YA TECHNO MALEWA VOLUME 2.
Title : MIKOSI KAMA INAMUANDAMA WERRA HIVI.
Description : WERRASON NGIAMA MAKANDA. Mfalme wa msitu ambaye pia ni kiongozi wa kundi la Wenge musica maisom mere (WMMM) Werraso Ngiama Makanda ama '...
Rating : 5