
Michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup)
mzunguko wa pili unaendelea leo kwa mchezo mmoja kuchezwa mmoja katika
uwanja wa Majimaji mjini Songea kati ya JKT Mlale dhidi ya Mighty
Elephant.
Kesho Jumatano kutakua
na michezo miwili, Kariakoo ya Lindi watawakaribisha Mshikamano FC
katika uwanja wa Ilulu – Lindi, Disemba 24 Njombe Mji watakua wenyeji wa
Green Warriors katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, na Pamba FC
watacheza dhidi ya Alliance uwanja wa CCM Kirumba.
Ijumaa siku ya sikukuu ya Krisamsi Lipuli FC watawakaribisha Kurugenzi katika uwanja wa Wambi Mafinga.
Mzunguko
huo wa pili unatarajiwa kumalizika Disemba 29 mwaka huu kwa michezo
minne, Wenda FC v Kimondo (Sokoine), Mji Mkuu (CDA) v Singida United
(Jamhuri), Mvuvuma v JKT Kanembwa (Tanganyika), Abajalo FC v Villa Squad
(Karume)
Timu saba za Ashanti United,
Burkinafaso, Geita Gold, Friends Rangers, Madini FCM, Panone na Rhino
Rangers zimeshakata tiketi ya kucheza mzunguko wa tatu wa Kombe la FA
mwezi Januari 2016, pamoja na timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.
Bingwa
wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup)
ataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC)
mwaka 2017.