Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Zanzibar Kassim Haji Salum Klabu za
Kenya Gor Mahia na KCCA ya Uganda ni miongoni mwa Timu zitakazocheza
Mashindano ya kugombea Mapinduzi Cup huko Zanzibar.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Januari 2.
Pamoja naTimu hizo 2 za nje Klabu kutoka Tanzania Bara ambazo zitashiriki ni Yanga, Simba, Azam FC na Mtibwa Sugar.
Kutoka Zanzibar ni Mafunzo na JKU.
Michuano hii ya Mapinduzi Cup ni dimba safi kwa Timu za Yanga, Azam
FC, JKU na Mafunzo ambazo zitashiriki Mashindano ya CAF ya Klabu Barani
Afrika.
Yanga watacheza michuano ya CAF CHAMPIONZ LIGI kwa kucheza mtoano
na Cercle de Joachim ya Mauritius wakati Azam FC wapo Kombe la
Shirikisho na watacheza na Mshindi kati ya Klabu ya Seychelles na
Bidvest Wits ya Afrika Kusini.
Mafunzo wao watacheza na AS Vita ya Congo DR kwenye CAF CHAMPIONZ
LIGI na JKU kucheza Kombe la Shirikisho na Gaborone United ya Botswana.