Pamoja na Tottenham kuonyesha nia ya kumnasa raia wa Algeria, Riyad Maherez, Manchester United nayo imeingia vitani.
United inaonekana kuvutiwa na kiungo huyo Mualgeria ambaye sasa ana mabao 14.
Hata hivyo klabu yake ya Leicester City imekuwa ikisisitizwa hatauzwa wakati wa dirisha dogo.
Lakini inaonekana timu zenye fedha zinaamini nguvu ya “mkwanja”.