Msaidizi mkuu wa kiongozi wa Korea
Kaskazini Kim Jong-un amefariki katika ajali ya barabarani, shirika la
habari la serikali la KCNA amesema.
Kim Yang-gon, 73, alikuwa katibu wa chama tawala cha Wafanyakazi na alisimamia uhusiano na Korea Kusini.
Alikuwa
kwenye ujumbe wa ngazi za juu kutoka Korea Kaskazini uliosaidia
kupunguza uhasama kati ya Pyongyang na Korea Kusini mwezi Agosti, baada
ya majeshi ya nchi hizo mbili kufyatuliana makombora.
Shirika la habari la KCNA lilimweleza kama rafiki mkuu wa Kim Jogn-un na mshirika mkuu wa mapinduzi.
"Rafiki Kim Yang-gon, katibu wa Chama cha Wafanyakazi na mwanachama
wa kamati kuu ya Politbureau... alifariki katika ajali ya barabarani saa
thenashara na robo asubuhi, Jumanne, akiwa na umri wa miaka 73," KCNA
ilisema, bila kutoa habari zaidi.
Shirika hilo limeongeza kuwa Kim Jong-un atahudhuria mazishi ya kiongozi huyo pamoja na maafisa 80 wakuu wa serikali.